Media

Worship with us

ONLINE STREAMING TIMES

SUNDAY: 07AM | 11AM

Thank you for joining us for our online worship experience. If you would like to view previous sermons kindly click the button below and explore our Sermons playlist from our YouTube channel. We encourage you to subscribe so as to receive timely updates and reminders for our next worship experience

We trust and believe that God is going to touch you as you worship with us

Get the App
VCC Mobile
Download Victory Christian Centre App. Search for VCCT in Play Store
Social Media Feeds
Facebook

Siku ya 11: Alhamisi, 21.3.2019

Somo: Usijisumbue, YUKO kazini

Tafakari: Kutoka 14:1-18
Mstari wa msingi: Kutoka 14:13

Wana wa-Israel walipokaribia bahari ya Shamu na majeshi ya Pharaoh yakiwafuatilia, ilionekana kama ndio mwisho wao. Hata hivyo, Mungu siku zote hutukomboa toka kwenye magumu.

"Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya."

Haijalishi unapitia magumu mangapi na ya ukumbwa gani, kumbuka kutojisumbua kwa sababu Mungu yuko kazini. Majitu unayoyaona leo,hautayaona tena.

Maombi Yako:
BWANA Yesu, Ninakataa kuchanganywa na mapito yangu. Kama ulivyojidhihirisha kwa Waisraeli katika bahari ya Shamu, nitakuona pia. Ameni.

Mch. Dkt. Huruma Nkone,
Mchungaji Kiongozi,
TAG-Victory Christian Centre Tabernacle.

Simu: 0762441719
Barua pepe: info@vcc.or.tz

Tunapenda sana kusikia kutoka kwako.Umejifunza nini kutoka kwenye tafakari ya leo #siku40katikaneno?
... See MoreSee Less

View on Facebook

Siku ya 10: Jumatano, 20.3.2019

Somo: Mtazame Yesu, si upepo

Tafakari: Mathayo 14:22-33
Mstari wa msingi: Mathayo 14:30-31

"Njoo". Yesu alisema maneno hayo akiwa amenyoosha wake kumpokea. Wanafunzi walimtazama Petro kwa umakini akitoka nje ya chombo na kuanza kutembea juu ya maji kumfuata Yesu. Awali Petro alimtazama Yesu lakini baadae alianza kutazama upepo uliomsababishia hofu.

Petro alipoanza tu kuogopa alianza kuzama, akapiga kelele akisema, "BWANA niokoe". Yesu alinyoosha mkono wake akamshika Petro kabla hajazama kabisa.

Petro alianza kuzama mara alipoelekeza macho yake kwenye upepo tofauti na awali alipokuwa akitembea juu ya maji akimtazama Yesu.

Masumbufu huanza unapotoa macho yako kwa Yesu. Upepo waweza kuwa chochote kinachoya tesa maisha yako, fedha, ndoa, kazi, afya n.k. Ukimtazama Yesu utatembea juu ya upepo wa Bahari.

Maombi yako:
BWANA, ninakutazama wewe tu, mwanzilishi na mtimilizaji wa imani yangu. Nisaidie kutokuamini kwangu ili nisije kuwa wa nia mbili. Amen.

Mch. Dkt. Huruma Nkone,
Mchungaji Kiongozi,
TAG-Victory Christian Centre Tabernacle.

Simu: 0762441719
Barua pepe: info@vcc.or.tz

Tunapenda sana kusikia kutoka kwako.Umejifunza nini kutoka kwenye tafakari ya leo #siku40katikaneno?
... See MoreSee Less

View on Facebook

Siku ya 9: Jumanne,19 Machi 2019

Somo: Mnara wa Babeli

Tafakari: Mwanzo 11:1-9
Neno kuu: Mwanzo 11:6

Mara tu baada ya Mungu kuadhibu ulimwengu kwa gharika na Nuhu na familia yake kuokoka, Mungu alikusudia wazaane, wakaongezeke na kuijaza nchi (Mwanzo 9:1). Baadae, wao wakaamua kujijengea mji wao na mnara, kujifanyia jina na kikubwa zaidi hawakutaka kutawanyika usoni pa nchi yote ambayo ilikuwa kinyume na mpango wa Mungu.

Mstari wa 6, tunasoma kuwa Mungu hakuafiki mpango huo hivyo akazimisha matamanio yao. Watu wana matamanio ya kufanikiwa hata kwa njia zilizo nje ya mpango wa Mungu.

Mungu aliona kujiinua kwao, na akazimisha mpango wao wa kujenga mnara kwa kuharibu mawasiliano yao.

Mungu anaona nia zetu. Ni maombi yangu kwamba nia zetu ziwe sawasawa na mpango wa Mungu. Jitathmini, ni mangapi unafanya yanaonekana sahihi au ya kujenga lakini nia uliyonayo sio njema (sio ya ki-Mungu)?

Maombi:
Mungu wangu, Asante kwa nguvu ya neno lako. Nisaidie kujua na kuuishi mpango wako. Ninatubu kwa kwenda kinyume na mpango wako mara kadhaa katika maisha yangu. Ninakataa roho ya kujikweza inayozuia utimilifu wa kusudi lako maishani mwangu. Kuanzia sasa ninakiri mwanzo mpya kwa jina la Yesu. Ameni.

Mch. Dkt. Huruma Nkone,
Mchungaji Kiongozi,
TAG-Victory Christian Centre Tabernacle.

Simu: 0762441719
Barua pepe: info@vcc.or.tz

Tunapenda sana kusikia kutoka kwako.Umejifunza nini kutoka kwenye tafakari ya leo #siku40katikaneno?
... See MoreSee Less

View on Facebook

Would you like to be mentored in one of those areas? If yes, kindly join with your fellow youth for a special mentorship program that will start tomorrow going onwards ... See MoreSee Less

View on Facebook

Siku ya 8:Jumatatu, 18 Machi 2019

Somo: Nguvu ya Neno la Mungu

Tafakari:
2 Timotheo 3:16-17

Biblia ni zaidi ya wino na karatasi. Maandiko yana pumzi ya Mungu.
Mwanzo 2:7 husema; "..... akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. Kama nafsi ya mtu ilivyo hai, maandiko nayo yana pumzi hivyo yana uhai.

Joshua aliagizwa alitafakari mchana na usiku neno la Mungu lililo hai. Ndio sababu tunatoa maneno na vifungu vya Biblia kila siku ila kila mtu atafakari. Jitendee wema kwa kusoma na kutafakari. Mguso utakaopata kupitia neno utakupa shuhuda.

Maombi yako
BWANA Yesu, nimekuwa sina muda mzuri wa kutafakari neno. Ninatubu kwa hilo. Sema nami kupitia Neno lako lililo hai. Ameni.

Mch. Dkt. Huruma Nkone,
Mchungaji Kiongozi,
TAG-Victory Christian Centre Tabernacle.

Simu: 0762441719
Barua pepe: info@vcc.or.tz

Tunapenda sana kusikia kutoka kwako.Umejifunza nini kutoka kwenye tafakari ya leo #siku40katikaneno?
... See MoreSee Less

View on Facebook
Twitter

Today we start our journey towards #40DaysInTheWord. In the next 39 days we will be sharing daily devitionals from different texts in the Bible. Kindly join us and remember to share with your circle

Load More...
Our Services

Our Services

Sunday

0700hrs - 0900hrs - First Service

0915hrs - 1045hrs - Second Service*

*Special teenagers service takes place concurrently in the teenagers' church

1100hrs - 1300hrs - Third Service

Tuesday

1730hrs - 1930hrs - Youth Service

Wednesday

1700hrs - 1900hrs - Women's Service

1730hrs - 1930hrs - Men's Fellowship*

*takes place only on the first and third Wednesday of the month

Friday

1700hrs - 1900hrs - Whole Church Prayers

Events / Calendar